Kamati ya siasa Wilaya ya Mtwara ikiambatana na Mkuu wa Walaya imefanya ziara ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo katika Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara.Jumla ya miradi 7 yenye thamani ya Tsh 3,292,448,361 ilikaguliwa. Miradi hiyo ni pamoja na ujenzi wa Shule ya Sekondari Mkunwa wenye thamani ya Tsh 470,000,000 pesa zilizopokelewa kutoka program ya SEQUIP, mradi wa Barabara Nanguruwe – Mkunwa yenye umbali wa Kilomita 1.7 wenye thamani ya Tsh 947,139,000 pesa kutoka Serikali kuu, mradi wa Bweni la watu wenye ulemavu shule ya Msingi Nanguruwe wenye thamani ya Tsh 100,000,000 pesa zilizopokelewa kutoka Serikali kuu, mradi wa maji Mitambo Msimbati wenye thamani ya Tsh 1,570,759,861 pesa zilizopokelewa kutoka program ya Ep4r, mradi huu utawezesha upatikanaji wa maji ndani ya vijiji 7 ambavyo ni Mitambo, Msimbati , Mnuo, , Luvula Litembe, Mtandi na Mngoji. Mradi wa Zahanati ya Mngoji wenye thamani ya Tsh 100,000,000 pesa zilizopatikana kutoka TPDC. Mradi mwengine ni mradi wa kikundi cha vijana kilichopatiwa mkopo wa Tsh 14,000,000 ukiwa ni mkopo wa asilimia 10 pesa zinazotolewa na Halmashauri na mradi wa mwisho ni mradi wa ujenzi wa visima viwili vya kuvuna maji ya mvua Msangamkuu wenye thamani ya Tsh 14,000,000 pesa zilizotolewa na mfuko wa maendeleo ya jamii Tasaf.
Aidha akiongea mbele ya wananchi Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Mtwara Ndg Nashiri Pontia alisema ziara hii ni matakwa ya kisheria ndani ya chama ikiwa na lengo la kupata uwelewa wa pamoja kwenye miradi inayotekelezwa ndani ya Halmashauri. Mwisho akifananisha na Halmashauri zingine alipongeza na kuridhika na utendaji kazi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara
Mtwara.
Anuani ya posta: 528.
Simu ya Mezani: 023-2333928
Simu: 023-2333928
Barua pepe: dedmtwara@mtwaradc.go.tz
Copyright ©2023 MTWARA DC . All rights reserved.