• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali |
    • Barua Pepe |
Mtwara District Council
Mtwara District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Elimu ya sekondari
      • Elimu Msingi
      • Usafi na Mazingira
      • Maji na Umwagiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Kazi na Kikosi cha Zima Moto.
      • Maendeleo ya Jamii,Jinsia na Vijana
      • Ardhi,Maliasiri na Mazingira
      • Utawala
      • Mipango,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Kililmo na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
    • Vitengo
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Uchaguzi
      • Kitengo cha Ugavi
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Habari na Mawasiliano.
    • Kamati za Halmashauri
      • Kamati ya Elimu,Afya na Maji
      • Kamati ya Fedha,Utawala na Mipango
      • Kamati ya Uchumi,Kazi na Mazingira
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Uwekezaji
    • Agriculture
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Huduma za kijamii
    • Huduma za Kifedha
    • Usambazaji Nishati ya Umeme
    • Maji
  • Madiwani
    • Kata ya Nanguruwe
    • Kata ya Mbawala
    • Kata ya Naumbu
    • Kata ya Ziwani
    • Kata ya Libobe
    • Kata ya Mayanga
    • Kata ya Ndumbwe
    • Kata ya Dihimba
    • Kata ya Mkunwa (HQ)
  • Miradi
    • Miradi Mpya
      • On going Project
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Utaratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Fomu
    • Zabuni
    • Newsletter
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Tukio

Livestock and Fisheries

IDARA YA MIFUGO NA UVUVI

1.0    UTANGULIZI
Idara ya mifugo na uvuvi inashughulikia utoaji wa elimu kwa wafugaji pamoja na kusimamia maendeleo ya shughuli za ufugaji na uvuvi kwa lengo la kuboresha sekta hiyo kuanzia ngazi ya Kijiji hadi Wilaya. Idara hii imegawanyika katika vitengo viwili ambavyo ni Mifugo na Uvuvi.
2.0    Sekta ya Mifugo
Miongoni mwa shughuli za kiuchumi na za kujipatia kipato za wakazi wa Halmashauri ni pamoja na shughuli za ufugaji. Sekta ya mifugo ni miongoni mwa sekta zinazochangia pato la ndani la halmshauri yetu kupitia ushuru wa nyama na wanyama wasafirishwao sehemu mbambali ndani na nje ya Wilaya.
2.1.0 Mifugo inayopatikana kwenye wilaya ya mtwara
Mifugo inayofugwa kwenye halmashauri ni kama inavyoonekana kwenye jedwali hapo chini;
Na. 1: Aina ya mifugo na idadi yake

Ng’ombe 3041, Mbuzi 29020, Kondoo 2018, Kuku  119756, Nguruwe 351, Bata 2206, Sungura Wawili (2), Kanga 592, Njiwa 1565, Mbwa 872 na Paka 1318.
2.2.0    Eneo lilotengwa kwa malisho.
Katika kuboresha maendeleo ya mifugo ndani ya wilaya, Halmashauri imetenga jumla ya Ha 1,187.94 katika kata za Mahurunga, Tangazo, Mbawala, Ndumbwe na Madimba kwaajili ya malisho ya mifugo kama inavyoonekana katika jedwali hapo chini:
Na. 2: maeneo yaliyotengwa kwaajili ya malisho
Kata ya Mahurunga;
    Marunga 27.97, Kihimika 92.56, Kitunguli 60.66
Kata ya Tangazo;
    Kilambo 252.83
Kata ya Mbawala;
    Makome 414.50
Kata ya Ndumbwe;
    Mbuo 3.93, Mnyundo 22.96
Kata ya Madimba;
    Mtendachi 312.55
Pia Halmashauri imekuwa ikishirikiana nawadau mbalimbali katika kuwawezesha wafugaji katika swala zima la ufugaji bora na kuwapatia miradi mbalimbali ya mifugo kama vile Ng’ombe, Mbuzi na kuku. Wafadhiri hao ni Concern, Africare,Tasaf na DADPS, Kutokana na miradi hiyo wananchi wameendelea kuboreka na kujipatia kipato na kuendesha maisha yao.
Halmashauri kushirikiana na wadau mbalimbali imepambana na kuzuia magonjwa mbalimbali ya mlipuko wa mifugo kama vile kideri na kichaa cha mbwa kwa kuwawezesha kuwachanjia mifugo yao hadi kufikia sasa uweneaji wa magonjwa hayo umepungua kwa kiasi kikubwa sana.
2.3.0    Ukusanyaji wa mapato
Idara kupitia kitengo cha mifugo imendelea kutoa elimu na kusimamia ukusanyaji wa mapato yatokanayo na mazao ya mifugo hususani ushuru wanyama namifugo iuzwayo ikiwa hai.
2.4.0 Uundwaji wa vikundi vya Mifugo
Miongoni mwa mikakati ya kuboresha na kuendeleza sekta ya Mifugo, ni pamoja na kuwezesha uundwaji wa vikundi vya Mifugo na kuvisajili ili kuviwezesha kupata fulsa mbalimbali ikiwemo mikopo na kuweza kukopa katika taasisi za kifedha na Idara ya Maendeleo ya Jamii . Pia kitengo cha mifugo kimeendelea kuwashawishi wafugaji kuunda vikundi mbalimbali vya ufugaji na kufuga ili kuwawezesha kujiongezea kipato.
2.5.0 Mikakati ya kuendeleza Sekta ya Mifugo
•    Mikakati iliyopo kwenye Halmashauri Wilaya ya Mtwara ni Kuwezesha umaliziaji wa ujenzi ya machinjio katika kata ya Mpapura, ukarabati wa majosho 4 ya mifugo katika vijiji vya Lilido, Mbawala, na Tangazo.
•    Kuhamasisha na kuhakikisha kila mwananchi anakinga mifugo yake dhidi ya magonjwa mbalimbali
•    Kuwatambua na kuwapa elimu wachinjaji wa mifugo ili shughuli zao zifanyike kitaalam na kuongeza kipato kwa kila mfugaji na kurahisisha ukusanyaji wa mapato ya Halmashauri.
3.0 Sekta ya Uvuvi
Miongoni mwa shughuli za kiuchumi na za kujipatia kipato kwa wakazi wa Halmashauri ni pamoja na shughuli za uvuvi. Ukanda wa bahari uliopo katika halmashauri yetu zinapofanyika shughuli za uvuvi unakadiriwa kufikia Kilomita 147. Sekta ya uvuvi ni miongoni mwa sekta zinazochangia pato la ndani la halmshauri yetu kupitia ukataji wa leseni, ushuru wa mazao ya bahari na faini na adhabu mbalibali. Sekta hii pia inatoa ajira kwa wananchi wanaoishi katika mwambao wabahari na hivyo kuijpatia kipato na kuweza kujikimu kimaisha.
3.1.0    Uhifadhi wa mazingira yaBahari
Sekta ya Uvuvi inaendelea kusimamia uhifadhi wa mazingira ya bahari kwa kutoa elimu ya ufahamu kwa jamii za wavuvi juu ya madhara yanayoweza kusababishwa na uharibifu wa mazingira kiikolojia na kiuchumi pia.
3.2.0    Ukusanyaji wa Maduhuli
Sekta ya uvuvi imekuwa ikiendelea na mikakati ya kukusanya maduhuli yanayotokana na shughuli za uvuvi.  Mpaka sasa sekta imevuka lengo la ukusanyaji la mwaka wa fedha 2016/17 kwa asilimia tano (5%) zaidi.
3.3.0    Udhibiti wa uvuvi haramu
Hali ya uvuvi haramu wa kutumia baruti imekuwa ikipungua siku hadi siku kutokana na kufanyika kwa doria mbalimbali katika maeneo yetu. Matamko namaagizo ya mkuu wa Wilaya katika mapambano dhidi ya uvuvi haramu yamesaidia sana kudhibiti uvuvi haramu.
3.4.0    Utekelezaji wa sheria ya Uvuvi
Shughuli nzima za usimamizi wa rasilimali ya uvuvi unafanywa kwa kufuata sheria na kanuni za uvuvi. Elimu juu ya ufuataji wa sheria katika uvunaji wa mazao ya bahari ikiwa ni pamoja na biashara ya mazao ya samaki inaendelea kutolewa kwa jamii ya wavuvi na wafanyabiashara wa mazao ya bahari.

3.5.0    Ushirikishwaji wa Rasilimali wa jamii ya Wavuvi
Wadau mbalimbali ikiwa ni pamoja na jamii ya wavuvi wanashirikiana kwa pamoja na halmashauri katika usimamizi shirikishi wa rasilimali ya bahari kupitia BMU (Beach management Units). Hizi ni taasisi ambazo kupitia uwezeshwaji wa WWF wana majukumu ya kuhifadhi mazingira ya bahari, kusimamia maendeleo ya sekta ya uvuvi katika vijiji vyao na majukumu mengineyo wanayopewa na ofisi ya uvuvi. Mpaka sasa tuna jumla ya BMU 11 zilizo hai katika kata ya Naumbu na Msangamkuu.
3.6.0    Ufugaji wa viumbe hai vya majini
Ufugaji wa viumbe hai vya majini unaendelea vizuri ambapo idadi ya wananchi na mabwawa mapya ya ufugaji wa samaki na mwani yanaongezeka. SWISSAID inaendelea kuwezesha mradi wa ufugaji wa samaki aina ya Mwatiko katika Kata ya Naumbu, Ndumbwe na Msimbati.
3.7.0    Ukusanyaji wa takwimu za Uvuvi
Takwimu za uvuvi ni miongoni mwa kipengele muhimu sana katika kuwezesha tathmini ya hali ya sekta ya uvuvi kiwilaya na kitaifa kwa ujumla. Shughuli hii ya ukusanyaji takwimu za uvuvi inaendelea vizuri.
3.8.0    Uundwaji wa vikundi vya Uvuvi
Miongoni mwa mikakati ya kuboresha na kuendeleza sekta ya Uvuvi, ni pamoja na kuwezesha uundwaji wa vikundi vya uvuvi na ufugaji wa viumbe hai na kuvisajili ili vipate mikopo na kuweza pia kukopesheka na taasisi za kifedha. Sekta ya uvuvi inaendelea kushawishi uundwaji wa vikundi vya wavuvi na wafugaji katika kata zote zinazojihusisha na shughuli za uvuvi katika wilaya yetu.
3.9.0    Mikakati ya kuendeleza sekta ya Uvuvi
Mikakati iliyopo kwa sasa ni pamoja na Kuwezesha vikundi kumi vya uvuvi kwa zana bora za uvuvi katika kata za Naumbu, Msimbati, Tangazo, na Ndumbwe, Kujenga soko la samaki katika kata ya Msangamkuu na kufanya shughuli za usimamizi na ufuatiliaji wa miradi ya uvuvi ifikapo juni 2017.

Responsibilities of Livestok and Fisheries Department in Mtwara DC

  • Visiting breeders to provide expert advice in their areas of work.

  • Providing vaccines against rabies and cats.

  • Inspects meat in abattoirs to be found in the Mtwara District after slaughtering every day.

  • Provide veterinary and make a diagnosis.

  • Review the health of livestock and livestock products

  • Diagnosis of diseases, monitoring and prevention

  • Provide advice and better education on animal

  • Develop department reports monthly, quarterly and annual

  • Monitor and implement development projects and council ward

  • Make the identification and registration of livestock and livestock statistics updating

  • Manage the Fisheries Act number 22 of 2003 and its regulations in 2009.

  • Provide a modern education on aquaculture

Matangazo

  • TANGAZO LA MAFUNZO UBORESHAJI WA DAFTARI KWA WALIOFAULU USAILI January 18, 2025
  • TANGAZO LA KAZI KUKIMBIZA MWENGE WA UHURU April 11, 2025
  • KUITWA KWENYE USAILI DAFTARI LA MPIGA KURA 2024 January 09, 2025
  • TANGAZO LA UCHAGUZI September 16, 2024
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • MHE. SAWALA AWATAKA WAFANYAKAZI WA MTWARA KUIPENDA MTWARA

    May 01, 2025
  • DED KAFUNDA AWAASA MAAFISA WAANDIKISHAJI WASAIDIZI NGAZI YA KATA KWENDA KUFANYA KAZI KWA WELEDI

    January 22, 2025
  • KATIBU WA CCM MKOA WA MTWARA APONGEZA USIMAMIZI WA MIRADI YA ZAIDI YA MILIONI 800 MTWARA DC

    January 07, 2025
  • KATIBU WA CCM MKOA WA MTWARA APONGEZA USIMAMIZI WA MIRADI YA ZAIDI YA MILIONI 800 MTWARA DC

    January 07, 2025
  • Angalia Zote

Video

RC Mtwara ataka mabadiliko Ligula Hospitali
Video zaidi

Kurasa za Haraka

  • New Projects
  • Speeches
  • Organizational Structure
  • Tenders
  • Applications Forms

Kurasa Mashuhuri

  • Tanzania Government Website
  • PO-RAG
  • Public Service Management
  • Mtwara Region Office
  • Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma
  • Tovuti ya Ikulu

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Sehemu

Wasiliana nasi

    Mtwara.

    Anuani ya posta: 528.

    Simu ya Mezani: 023-2333928

    Simu: 023-2333928

    Barua pepe: dedmtwara@mtwaradc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Usiri
    • Kanusho
    • Maswali
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Copyright ©2023 MTWARA DC . All rights reserved.