Yamejiri hayo leo Mei Mosi 2025, Wilayani Newala katika maadhimisho ya siku ya Wafanyakazi Duniani yaliyofanyika Kimkoa katika Kiwanja cha Saba Saba Newala.
Aidha amekumbusha kuendelea kutoa huduma bora kwa kuzingatia Sheria na Miongozo, pamoja na kuipenda Mtwara kwani mkoa wa Mtwara unaupungufu wa watumishi kwa zaidi ya Asilimia 40. "Upande wa Serikali tunawahakikishieni kuendelea kuweka mazingira rafiki kwa Watumishi" Alisema Mkuu wa Mkoa huyo.
Hata hivyo amewataka Wafanyakazi kuendelea kudumisha amani kwani kwenye amani ndio kwenye maendeleo. "Kundi lolote litakalo eneza propaganda za uvunjifu wa amani tulipuuze" aliongeza Mhe. Sawala
Kuelekea Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Mwezi Oktoba 2025 amewahasa Watumishi wenye nia ya kugombea nafasi mbalimbali kufuata Miongozo.
Aidha Kauli Mbiu ya Siku ya Wafanyakazi Duniani Mwaka huu inasema"Uchaguzi Mkuu 2025 utuletee Viongozi Wanaojali Haki na Maslahi ya Wafanyakazi, Sote Tushiriki"
Mtwara.
Anuani ya posta: 528.
Simu ya Mezani: 023-2333928
Simu: 023-2333928
Barua pepe: dedmtwara@mtwaradc.go.tz
Copyright ©2023 MTWARA DC . All rights reserved.