IDARA YA MIPANGO, TAKWIMU NA UFUATILIAJI
1.0 UTANGULIZI;
Idara ya Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji ni kiungo cha Idara zote katika Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara. Idara hii inahusika katika usimamizi wa uandaaji wa Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP), maelezo mafupi ya Halmashauri, (Social profile), maelezo mafupi ya uwekezaji (Investment Profile) pamoja na Mpango na Bajeti ya kila mwaka. Idara pia inahusika katika Ukusanyaji na uchambuzi wa Takwimu mbalimbali za kiuchumi na kijamii katika Halmashauri ya Wilaya. Aidha, utekelezaji wa mpango na bajeti kwa kila mwaka husimamiwa na idara hii kwa kushirikiana na Idara zote. Idara hii inaongozwa na Afisa Mipango wa Wilaya na imegawanyika katika sehemu tatu kama ifuatavyo:-
MAJUKUMU MUHIMU YA IDARA.
Idara ya Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji ina jukumu la kuratibu utoaji wa taarifa mbalimbali za maendeleo za Wilaya kwa Viongozi wa ngazi za Kitaifa, Kimkoa, Wilaya na wadau wa maendeleo, pamoja na kazi zingine za kawaida ina majukumu muhimu yafuatayo;
3.0 ORODHA YA WATUMISHI
Idara ina jumla ya watumishi 04 kama ifuatavyo:-
Mkuu wa Idara 1
Wachumi 2
Mtakwimu 1
TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO KWA BAJETI YA MWAKA 2016/2017.
A: UTANGULIZI,
Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara ilipanga kukusanya na kutumia jumla ya shilingi 6,818,086,000.00 katika kutekeleza miradi ya maendeleo kwa kipindi cha mwaka wa fedha wa 2016/2017. Sawa na asilimia 23.6 ya bajeti nzima ya Halmashauri ya Wilaya inayofikia shilingi 28,770,100,000.00
Mchanganuo wa fedha hizo za maendeleo na vyanzo vyake ni kama unavyoonekana katika jedwali hapa chini:-
NA
|
CHANZO
|
KIASI |
% |
1
|
Mapato ya ndani (Own Source)
|
1,334,956,000.00 |
17.6 |
2
|
Ruzuku serikali kuu
|
5,440,130,000.00 |
81.7 |
3
|
Wadau wa maendeleo
|
43,000,000.00 |
0.7 |
|
JUMLA
|
6,818,086,000.00 |
100.0 |
B: MAPATO,
Halmashauri ya Wilaya imeshapokea kiasi cha shilingi 5,917,546,329.58 sawa na asilimia 78.3 tu ya makisio ya mwaka 2016/2017 zikiwa ni kwa ajili ya kunusuru Kaya maskini (TASAF III), Maji, Mfuko wa barabara, UNICEF na LGCDG.
C: MATUMIZI,
Hadi sasa kiasi cha shilingi 4,877,939,074.57 kimeshatumika kugharamia miradi mbalimbali inayoendelea kutekelezwa katika Halmashauri ya Wilaya Mtwara.
D: UTEKELEZAJI,
Na |
SEKTA |
JINA LA MRADI |
HALI YA UTEKELEZAJI |
01.
|
Elimu ya Sekondari
|
Ujenzi wa vyumba vya maabara 33
|
Ujenzi wa vyumba vya maabara katika shule za Sekondari 11 upo katika hatua ya umaliziaji.
|
Utengenezaji wa madawati
|
Jumla ya madwati 900 yametengenezawa na kuyapeleka katika shule zote za sekondari.
|
||
Ujenzi wa matundu ya vyoo.
|
Ujenzi wa matundu ya vyoo 10 katika shule ya sekondari Libobe na 10 Ndumbwe umefanyika.
|
||
Ujenzi wa vyumba vya madarasa
|
Ujenzi wa vyumba 2 vya madarasa katika sekondari ya Madimba unaendelea.
|
||
02.
|
Elimu ya Msingi
|
Ujenzi wa vyumba vya madarasa
|
Ujenzi wa vyumba vya madarasa 8 umekamilika katika shule ya Mbawala na madarasa 3 katika shule za msingi Mnomo, Ilala na Nanyati unaendelea.
|
Utengenezaji wa madawati
|
Jumla ya madawati 200 yametengenezwa.
|
||
Ujenzi wa matundu ya vyoo
|
Ujenzi wa matundu ya vyoo 18 umekamilika katika shule ya Mbawala na matundu 15 katika shule za Mnete, Utende na Kitunguli unaendelea.
|
||
Ujenzi wa nyumba za walimu
|
Ujenzi wa nyumba ya mwalimu katika shule ya msingi Mtandi umekamilika.
|
||
03.
|
Afya
|
Ujenzi wa Zahanati mpya
|
Ujenzi wa nyumba 4 katika OPD mpya zilizo katika vijiji vya Makome A, Makome B, Mtama na Nanyani upo katika hatua za awali.
|
|
Ujenzi wa OPD katika vijiji vya Mbuo, Mngoji na Likonde unaendelea.
|
||
04.
|
Maji
|
Mradi wa maji Msangamkuu
|
Ukamilishaji wa ujenzi wa mradi huu unaendelea na umefikia asilimia 85 ya ukamilishaji.
|
Mradi wa maji Kilambo
|
Ukamilishaji wa ujenzi wa mradi huu unaendelea na umefikia asilimia 85 ya ukamilishaji.
|
||
Mradi wa maji Mpapura - Lyowa
|
Ukamilishaji wa ujenzi wa mradi huu unaendelea na umefikia asilimia 70 ya ukamilishaji.
|
||
Mradi wa maji Mayaya
|
Ukamilishaji wa ujenzi wa mradi huu unaendelea na umefikia asilimia 70 ya ukamilishaji.
|
||
05.
|
Barabara
|
Matengenezo ya dharura ya barabara
|
Ujenzi wa kalvati mistari minne pamoja na kuta na mikono ya kalvati imejengwa katika barabara ya Chekeleni – Mkonye hadi Mtama, kazi imekamilika.
|
Ujenzi wa daraja
|
Uchimbaji wa msingi wa daraja,ujenzi wa nguzo tatu za daraja,ujenzi wa kuta za mikono ya daraja na kumimina zege la deki ya daraja katika barabara ya Namuhi-Mnyija kazi imekamilika.
|
||
06
|
Kilimo
|
Ujenzi wa bwawa na mifereji ya umwagiliaji
|
Ujenzi wa bwawa na mifereji ya umwagiliaji katika mradi wa umwagiliaji Kitere unaendelea na umefikia asilimia 95 ya ukamilishaji.
|
07
|
Mfuko wa Jimbo
|
Ununuzi wa saruji
|
Mifuko 2,050 ya saruji imenunuliwa kwa ajili ya kuendeleza miradi ya maendeleo, saruji imeshapelekwa
|
08
|
TASAF
|
Kusaidia kaya 10,449 kujikwamua na umaskini
|
Jumla ya kaya 10,129 maskini zimewezeshwa na jumla ya Tsh 1,361,699,650.40 zimetumika.
|
09
|
Maendeleo ya Jamii
|
Kuwezesha utoaji wa mikopo
|
Jumla ya vikundi 33 vya wanawake na vijana vimepewa mkopo wa jumla ya Tsh 62,740,000 kutoka kwenye vyanzo vya ndani vya mapato ya Halmashauri
|
Responsibilities of Planning, Monitoring and Statistics Department in Mtwara DC
Coordinate the activities of the Council budget preparation
Coordinate the preparation of the implementation of the strategic plan of the Council
Coordinate the activities of collection, analysis, and interpretation of the data handling various newspapers to make use especially in planning development projects.
Coordinate the activities of the implementation of the development projects of the District ventures, aviation projects
Prepare labels of various projects (project write ups) for the purposes of pointers to pray for funding from various donors.
Coordination of participatory community planning activities
Secretary of the committee of the Council Expert
Secretary of the Economic Committee, Construction and Environment
Coordinate the review of the reporting process of the District (District Profile) for example: Social Economic Profile, etc. Investment Profile
Coordinate the preparation of the action plan election manifesto with its reports on the implementation (of the half year and full year).
Provide advice on economic issues and raising the output of resident to strengthen modern agriculture and animal husbandry as well as other economic activities.
Mtwara.
Anuani ya posta: 528.
Simu ya Mezani: 023-2333928
Simu: 023-2333928
Barua pepe: dedmtwara@mtwaradc.go.tz
Copyright ©2023 MTWARA DC . All rights reserved.