A. Eneo
Halmashauri ya Wilaya Mtwara ni moja ya Halmashauri 9 za Mkoa wa Mtwara. Ipo kati ya longitudo 390 0 "na 400 27" mashariki ya Grinwichi. Pia uko kati ya latitudo 100 0" na 100 07” kusini mwa Ikweta. Imepakana na Bahari ya Hindi katika eneo la Mashariki, Lindi eneo la kaskazini, Msumbiji upande wa kusini na Mji wa Nanyamba upande wa magharibi. Ina jumla ya kilometa za mraba 3,597.
B. Idadi ya Wakazi.
Kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012, Halmashauri ya Wilaya Mtwara ilikuwa na idadi ya watu 127,623 ambao walikuwa 60,409 wanawake na wanaume 67,214 na kiwango cha ukuaji wa 1.4. Idadi kubwa ya ...kundi la wakazi ni Wamakonde.
C. Hali ya Hewa.
Mabadiliko ya Altitude ni kati kati ya 0 hadi 350 mita kwa usawa wa Bahari ya Hindi. Wilaya hii ina misimu miwili ya Hali ya hewa, msimu wa joto baridi mvua (Masika) ambao huanza Novemba hadi Mei na msimu wa hali ya ukavu na joto (kiangazi) kuanzia Juni hadi Oktoba. wastani wa mvua ni kati ya 800mm-900mm wakati nyuzijoto wastani ni kati ya 230 C katika Juni na 300 C katika Oktoba.
Wakati tunaelekea kuifahamu Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara ni vizuri tukajikumbusha historia fupi ya Mkoa wa Mtwara kwa ujumla ili msomaji wangu upate muunganiko ulio sahihi wa kulifahamu eneo lote la Mtwara vijijini.
1.1 HISTORIA FUPI YA MKOA WA MTWARA.
Mfumo wa utawala wa ukoloni uliigawa Tanzania katika majimbo Nane (8), Mkoa wa Mtwara ulikuwa ndani ya jimbo la Kusini ambalo lilijumuisha mikoa ya Mtwara, Ruvuma na Lindi
ambapo makao makuu ya jimbo yalikuwa Lindi.
Mkoa wa Mtwara ulianzishwa rasmi mwaka 1971 kutokana na Mpango wa Madaraka Mikoani
ambao ulilenga kusogeza huduma karibu zaidi na wananchi.
Mkoa huu ulipoanzishwa ulikuwa tayari na Wilaya tatu (3) ambazo ni Masasi iliyoanzishwa
mwaka 1928 chini ya ukoloni wa Kijerumani, Newala mwaka 1956 chini ya wakoloni wa
Kiingereza na Mtwara ilianzishwa mwaka 1961.
(a). HALMASHAURI YA WILAYA YA MTWARA.
Kwa sasa hivi Kiutawala Mkoa umegawanyika katika Wilaya 5 na Halmashauri 9 ambapo ndani yake utakutana na Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara, hadi kufikia katikati ya mwaka 2014 ilikuwa na idadi ya watu 234,563 katika Tarafa 6, Kata 28, Vijiji 157 na Vitongoji 638.
Kutokana na sababu za Kijiografia ukubwa wa eneo na kurahisisha huduma za msingi za wananchi yalifanyika mabadiliko ya kiutawala ambapo Halmashauri iligawanywa mwaka 2014 kabla ya uchaguzi wa serikali za mitaa na kuzaliwa Halmashauri ya mji wa Nanyamba. Tukio hili lilisababisha kupoteza baadhi ya maeneo ya kiutawala ambayo yalihamia katika mji na kuzaliwa maeneo mapya yaliyounganika na yale ya zamani kwahiyo hadi hivi sasa Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara ina jumla ya wakazi 127,623 kati yao wanaume ni 67,214 na wanawake 60,409 katika Tarafa 5, Kata 21 na Vijiji 110.
1.2 ASILI YA NENO MTWARA.
Neno Mtwara limetokana na neno la lugha ya Kimakonde “kutwala” ikiwa na maana ya
kuchukua (kunyakua) kitu chochote.
Mtwara ni Jina inalotumika kwa maana 3 tofauti zifuatazo:
• Mtwara jina la Mkoa.
• Mtwara jina la mji wa Makao Makuu ya Mkoa.
• Mtwara ni Wilaya na Makao Makuu ya Wilaya ambayo kiutawala ina Halmashauri 2,
ambazo ni Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara/Mikindani na Halmashauri ya Mtwara.
1.3 KABILA NA UTAMADUNI WA WAKAZI.
Asilimia kubwa ya Wakazi wa asili wa eneo hili ni wamakonde ambao wanatumia lugha ya kimakonde kama nyenzo ya mawasiliano, katika jamii ya kimakonde wamegawanyika katika sehemu mbili, sehemu ya kwanza ni wale wanaoishi katika Ukanda wa Pwani wanajulikana kama ”Wamalaba” na wale wanaoishi tofauti na ukanda wa pwani ” wamakonde wa bara” ingawa wanaongea lugha moja lakini kuna baadhi ya tofauti katika mfumo wao mzima wa maisha katika shughuli za kiuchumi, kijamii na desturi zao. Ukitaka kushuhudia haya unaweza kutembelea maeneo ya pwani kama vile Msangamkuu, Mgao, Nalingu, Msimbati na maeneo mengine yenye asili ya Pwani ambapo utakutana na vitu tofauti na sehemu za bara kama vile Mbawala, Kitere, Dihimba, Nanguruwe pamoja na sehemu zingine za Mtwara Vijijini.
1.4 SHUGHULI ZA KIUCHUMI.
Shughuli kuu za kiuchumi kwa wakazi wa eneo hili ni Kilimo kwa wakazi wengi wa Bara, Uvuvi kwa wakazi wanaoishi ukanda wa pwani na Ufugaji kwa kiasi kidogo kinafanywa na wananchi kutoka sehemu zote yaani bara na pwani. Zao kuu la biaashara ni korosho likifuatiwa na muhogo, Uvuvi na ufugaji wa kuku na mbuzi nao ni sehemu ya vyanzo vya kipato cha wakazi wa eneo hili hadi sasa.
2. UTAWALA
2.1 ORODHA YA WAKURUGENZI WATENDAJI KUANZIA MWAKA 1984 HADI SASA;
NA
|
JINA
|
MWAKA
|
1.
|
OMARI S. KWILEKA
|
1984 - 1985
|
2.
|
KAPINGA
|
1985 - 1986
|
3.
|
ANDREA CHIPATA
|
1986 - 1993
|
4.
|
MARTIN KANIKI
|
1993 - 1995
|
5.
|
MBWIGA K. MWALENDE
|
1995 - 2001
|
6.
|
ESTHER WAKARI
|
2001 - 2004
|
7.
|
HENRY UISO
|
2004 - 2007
|
8.
|
JAVIS A. SIMBEYE
|
2007 - 2011
|
9.
|
MOHAMED S. NGWALIMA
|
2011 - 2012
|
10.
|
IDDI I. MSHILI
|
2012 - 2014
|
11.
|
JULIUS M. KAONDO
|
2014 - 2015
|
12.
|
ZAKARIA N. NACHOA
|
2015 - 2016
|
13.
|
OMARI J. KIPANGA
|
2016 HADI SASA
|
Mtwara.
Anuani ya posta: 528.
Simu ya Mezani: 023-2333928
Simu: 023-2333928
Barua pepe: dedmtwara@mtwaradc.go.tz
Copyright ©2023 MTWARA DC . All rights reserved.