TAARIFA YA IDARA YA MAJI HALMASHAURI YA WILAYA MTWARA
HALI YA UPATIKANAJI WA HUDUMA YA MAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MTWARA
UTANGULIZI
Halmashauri ya wilaya ya Mtwara ina jumla ya vijiji 110 kwa idadi ya watu 127,440 (sensa 2012) kati ya watu hao 57,335 wanapata huduma ya maji safi na salama ni sawa na asilimia arobaini na tano (45%). Asilimia hamsini na tano (55%) ya watu waliobaki 70,105 hawapati maji safi na salama na hutembea umbali mrefu kutafuta maji kinyume na sera ya maji inayosema maji yapatikane kwa umbali usiozidi mita 400. Ifikapo mwaka 2020 huduma hii itaongezeka hadi kufikia asilimia 85% kutokana na miradi ya vijiji kumi inayoendelea na utekelezaji kupitia program ya kitaifa ya maji na usafi wa mazingira pamoja na ukarabati wa miradi isiyotoa huduma kutokana na kuchakaa kwa miundombinu yake.
Halmashauri ya wilaya ya Mtwara inategemea maji ya visima virefu, visima vifupi vyenye pampu ya mkono, teknolojia ya uvunaji maji ya mvua, mitandao ya miradi ya maji ya bomba na mabwawa.
HALI YA MIUNDOMBINU YA MAJI
Miradi ya iliyofungwa pampu imegawanyika katika sehemu mbalimbali ambavyo ni visima virefu na visima vifupi.
Ifuatayo ni hali ya miundombinu iliyopo katika halmashauri ya wilaya mtwara.
Na |
Aina ya Miradi |
Iliyopo |
Inayofanya kazi |
Isiyofanya kazi |
1
|
Visima virefu vyenye pampu ya mkono.
|
32 |
10 |
12 |
2
|
Visima vifupi vyenye pampu ya mkono
|
42 |
21 |
21 |
3
|
Mabwawa
|
2 |
2 |
0 |
4
|
Matenki ya kuvunia maji ya mvua.
|
235 |
135 |
100 |
5
|
Mtandao wa maji ya mabomba
|
20 |
13 |
7 |
Halmashauri ina jumla ya jumuiya za watumiaji maji (COWSO) 18 ambapo Jumuiya zote zimesajiliwa kisheria na kupatiwa vyeti. Jumuiya hizo ni
Halmashauri ya wilaya ya Mtwara ina jumla ya miradi ya maji 20 ya bomba ambayo imefungwa pampu ya umeme wa TANESCO/Solar pamoja na mechanical generator. Kati ya miradi hiyo miradi 13 imekwisha kamilika na miradi 7 iliyobaki ipo katika hatua mbalimbali za utekelezaji na ukamilishwaji.
Ifuatayo ni miradi iliyokamilika na inatoa huduma kwa jamii.
Ifuatayo ni miradi iliyopo katika hatua mbalimbali za ukamilishaji.
Mtwara.
Anuani ya posta: 528.
Simu ya Mezani: 023-2333928
Simu: 023-2333928
Barua pepe: dedmtwara@mtwaradc.go.tz
Copyright ©2023 MTWARA DC . All rights reserved.