Leo Jan 22, 2025 yameendelea mafunzo kwa maafisa waandikishaji wasaidizi ngazi ya kata, ambapo maafisa hao wamepata fursa ya kujifunza BVR kwa vitendo.
Nae Ndg. Abeid A. Kafunda Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara alitumia nafasi hii ya leo kuwaasa maafisa hao kuzingatia walichojifunza kwa siku zote mbili.
“Hakuna suala la kujiongeza twende tukafanye kazi kwa kufuata sheria, kanunu, utaratibu na miongozo ” alisema Kafunda
Aidha mafunzo hayo ya siku mbili yanatamatika leo Jan 22, 2025 katika ukumbi wa Chuo cha Ufundi VETA.
Mtwara.
Anuani ya posta: 528.
Simu ya Mezani: 023-2333928
Simu: 023-2333928
Barua pepe: dedmtwara@mtwaradc.go.tz
Copyright ©2023 MTWARA DC . All rights reserved.