Leo Sep 10, 2025 Katibu Tawala wa Wilaya ya Mtwara, Wakili. Richard Jackson Mwalingo amezindua rasmi zoezi la utoaji wa chanjo za ruzuku na utambuzi wa mifugo katika Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara.
Zoezi hilo limefanyika leo kwa kuchanja moja kwa moja na kuwatambua kwa kuwavesha Hereni N'gombe wa Kata ya Naumbu. Matarajio ya Halmashauri ni kuchanja na kutambua Ng'ombe zaidi ya 3,700 na Mbuzi zaidi ya 27,600.
Akiongea mbele ya wananchi mgeni rasmi wa zoezi hilo Wakili. Mwalingo alipongeza Serikali kwa kuchangia Chanjo hiyo kwa Asilimia 75 na Asilimia 100 kwa upande wa Hereni. Kitu ambacho kinaonesha namna gani Serikali inavyowathamini wafugaji.
Nae Kaimu Mkuu wa Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Dkt. Innocent Masawe alitoa faida ya Chanjo hiyo kuwa ni kumkinga mnyama na magonjwa na kumpunguzia mfugaji gharama za matibabu. Aidha mfugaji atachangia Sh. 300 kwa Mbuzi na Sh. 500 kwa Ng'ombe na kwa upande wa utambuzi Serikali tayari imeshagharamia.
Dkt. Innocent aliongeza kuwa pamoja na zoezi hilo tayari zoezi la uchanjaji wa kuku na Bata limeshafanyika ambapo zaidi ya kuku elfu Sabini na Tano wamepatiwa chanjo, Asilimia 15 hawakupatiwa chanjo kwa sababu chanjo zilizoletwa zilikuwa pungufu kutokana na changamoto ya takwimu, hivyo chanjo hizo zitakuja na kukamilisha Asilimia 15 zilizobaki.
Ikumbukwe kuwa zoezi hilo linaenda sambamba na uwekaji wa hereni za kielektroniki kwa ajili ya utambuzi wa mifugo, hatua inayolenga kuimarisha ulinzi wa mifugo na kusaidia wizara kuwa na takwimu sahihi za mifugo.
Mtwara.
Anuani ya posta: 528.
Simu ya Mezani: 023-2333928
Simu: 023-2333928
Barua pepe: dedmtwara@mtwaradc.go.tz
Copyright ©2023 MTWARA DC . All rights reserved.