• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali |
    • Barua Pepe |
Mtwara District Council
Mtwara District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Elimu ya sekondari
      • Elimu Msingi
      • Usafi na Mazingira
      • Maji na Umwagiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Kazi na Kikosi cha Zima Moto.
      • Maendeleo ya Jamii,Jinsia na Vijana
      • Ardhi,Maliasiri na Mazingira
      • Utawala
      • Mipango,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Kililmo na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
    • Vitengo
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Uchaguzi
      • Kitengo cha Ugavi
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Habari na Mawasiliano.
    • Kamati za Halmashauri
      • Kamati ya Elimu,Afya na Maji
      • Kamati ya Fedha,Utawala na Mipango
      • Kamati ya Uchumi,Kazi na Mazingira
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Uwekezaji
    • Agriculture
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Huduma za kijamii
    • Huduma za Kifedha
    • Usambazaji Nishati ya Umeme
    • Maji
  • Madiwani
    • Kata ya Nanguruwe
    • Kata ya Mbawala
    • Kata ya Naumbu
    • Kata ya Ziwani
    • Kata ya Libobe
    • Kata ya Mayanga
    • Kata ya Ndumbwe
    • Kata ya Dihimba
    • Kata ya Mkunwa (HQ)
  • Miradi
    • Miradi Mpya
      • On going Project
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Utaratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Fomu
    • Zabuni
    • Newsletter
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Tukio

Land,Natural Resources and Environment

TAARIFA YA IDARA YA ARDHI NA MALIASILI 

UTANGULIZI

Idara ya Ardhi na Maliasili inazo sekta za Ardhi  yenye vitengo vya Ardhi, Mipangomiji na vijiji, Uthamini  pamoja na Upimaji na Ramani, sekta ya Maliasili yenye vitengo vya Misitu, Ufugaji wa Nyuki, na Wanyamapori. Madhumuni makubwa ya Idara hii ni kusimamia matumizi endelevu ya Ardhi na Maliasili kwa manufaa ya kizazi cha sasa na vizazi vijavyo.

  • MAJUKUMU MUHIMU YA IDARA
  • Jukumu kubwa la idara ya Ardhi na Maliasili ni kulinda, kuhifadhi na kuboresha mazingira ya ukuaji na uendelezaji wa Miji katika Halmashauri yetu kwa kuendeleza rasilimali ardhi pamoja na  matumizi bora ya Ardhi kwa kutambua maeneo yaliyoiva kimji na kuandaliwa michoro ya mipango miji, kupima viwanja vya makazi na matumizi mengine pamoja na mashamba, kuandaa hati miliki za Ardhi kwa mujibu wa sheria za Ardhi Na. 4 na 5 za 1999, pamoja  na kutekeleza  sera ya Taifa ya ardhi ya 1995 na sera ya maendeleo ya makazi ya 2000. Pia sekta ya maliasili inashughulika na usimamiaji wa rasilimali za misitu kwa uendelevu wa vizazi vilivyopo na vijavyo,  na usimamizi wa sera na sheria za misitu pamoja na suala zima la ukusanyaji wa mapato ya Serikali kuu na Halmashauri.
  • ORODHA YA WATUMISHI NA MGAWANYO WA KAZI

 Idara ina jumla ya watumishi tisa wanaofanya kazi katika vitengo/sekta mbalimbali kama ilivyoainishwa hapa chini;

Na
Kada

Mahitaji

Waliopo

Upungufu

1.
Mkuu wa Idara

1

1

-

2.
Afisa Mipangomiji

2

2

-

3.
Afisa Ardhi

2

1

1

4.
Afisa Ardhi Msaidizi

1

-

1

5.
Mpima Ardhi

2

1

1

6.
Fundi Sanifu Upimaji

2

1

1

7.
Mthamini

2

1

1

8.
Mrasimu Ramani

1

-

1

  1. SHUGHULI ZILIZOTEKELEZWA MWAKA 2014/2015 HADI 2016/2017

Katika kipindi tajwa hapo juu idara imetekeleza shughuli mbalimbali kulingana na mpango kazi wake. Shughuli muhimu zilizotekelezwa ni pamoja na zifuatazo;

  • Kusimamia zoezi la ulipaji wa fidia ya mazao kwa wananchi wa vijiji vya Kilambo, Msimbati na Litembe ambapo kulikuwa na zoezi la utafiti wa gesi lililokuwa likifanywa na Kampuni ya M & P.
  • Kusimamia zoezi la uhamasishaji, uthamini na uandaaji wa michoro ya mipangomiji kwenye vijiji vya Kisiwa na Mgao ambapo Mamlaka ya Bandari Tanzania iko katika mchakato wa kutwaa ardhi kwa ajili ya ujenzi wa Bandari. Jumla ya ekari 593 zinatarajiwa kutwaliwa lakini hadi sasa zoezi hilo limesimama.
  • Kuandaa michoro ya mipangomiji katika eneo la viwanda Msijute ambapo tayari kazi ya kupima viwanja 380 vya matumizi ya viwanda na biashara imekamilika.
  • Kuandaa mipango ya matumizi bora ya ardhi katika vijiji vya Kilambo, Kihimika, Kitunguli, Mahurunga na Kivava kwa ajili ya mchakato wa kupewa ardhi mwekezaji Oyo Real Estate kwa ajili ya uwekezaji kwenye kilimo cha miwa. Baada ya vikao kwenye vijiji husika na wananchi kuridhia mwekezaji kupewa ardhi, maombi yaliwasilishwa kwenye Kamati ya Ugawaji Ardhi ya Wilaya ambapo ilipendekezwa apewe ardhi yenye ukubwa wa hekta 3,203.25 na maombi hayo yaliwasilishwa kwa Kamishna wa Ardhi ambapo aliridhia na tayari tangazo la kusudio la kuhaulishwa ardhi hiyo lilishabandikwa kwenye vijiji vyote ambapo ardhi itatwaliwa.
  • Kwa kushirikiana na Manispaa ya Mtwara Mikindani, Halmashauri imekamilisha kazi ya uandaaji wa mpango kabambe wa pamoja (Joint Master plan) ambapo mpango huo unahusisha eneo lote la Manispaa ya Mtwara Mikindani na eneo la Kata tisa za Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara ambazo ni Naumbu, Mayanga, Mkunwa, Mbawala, Nanguruwe, Ziwani, Moma, Msangamkuu na Nalingu. Tayari mpango huo umeshazinduliwa na kwa ajili ya utekelezaji na usimamizi wake.
  • Kuandaa na kuwasilisha viwango vya bei la soko la ardhi Ofisi ya Mthamini Mkuu wa Serikali kwa ajili ya kuandaa daftari la bei ya soko la kwa nchi nzima.
  • Kufanya upimaji wa mashamba 47 kwa ajili ya utoaji wa hati miliki za kimila katika kijiji cha Ndumbwe.
  • Kufanya uthamini wa njia ya Bomba la Maji kutoka mto Ruvuma kwa kushirikiana na Ofisi ya Katibu Tawala Mkoa pamoja na Wizara ya Maji.
  • Kufanya uthamini wa mali za kudumu za Halmashauri .
  • Kuandaa michoro ya mipangomiji kwenye maeneo mbalimbali yenye jumla ya viwanja 9,200.
  • Kupokea na kushughulikia kero mbalimbali zinazohusiana na masuala ya ardhi.
  • Kwa kushirikana na Wakala wa huduma za misitu Tanzania kupanda miti aina ya mitiki katika Msitu wa hifadhi wa Ziwani. Eneo la hekta 4.5 lilipandwa miti.
  • Sekta ya Misitu kwa kushrikiana na Wakala wa huduma za misitu iliendesha mafunzo kuhusu uhifadhi wa mikoko kwa kamati za vijiji vya Ndumbwe na Namgogoli.
  • Kupeleka mizinga kumi  ya serikali chini ya wakala wa huduma za misitu katika kijiji cha Msimbati na kuitundika katika  eneo la msitu wa mikoko litakalotumika kwa mafunzo ya ufugaji wa nyuki kwa vikundi vya wafugaji wa nyuki
  • Kushirikiana na wakala wa huduma za misitu kuongeza mawe madogo ya mpaka katika misitu ya akiba ya Naliendele na Ziwani ambapo jumla ya mawe 16 yalisimikwa katika msitu wa Naliendele na mawe 15 katika msitu wa Ziwani.
  • Kushirikiana na wakala wa huduma za misitu kusimamia upandaji miti katika msitu wa akiba wa Ziwani ambako mpaka mwisho wa mwezi machi jumla ya miti 5,700 aina ya mitiki na mielezi ilikuwa imepandwa.
  • MIKAKATI
  • Kuandaa Michoro ya Mipangomoiji yenye viwanja 10,000
  • Kuandaa mipango ya matumizi bora ya ardhi katika vijiji 12
  • Kuandaa hati miliki za kimila 2,000
  • Kupima viwanja vya matumizi mbalimbali 2,500
  • Kuandaa hatiza kumiliki ardhi zipatazo 2,000

Responsibilities of Land and Natural Resources Department in Mtwara DC

  • Coordinate and control the development of cities and villages.

  • Coordinate the preparation of plans for land use Rural and Urban.

  • Build capacity to plan and implement promotional duties on Council land.

  • To educate the public about plans to land use.

  • Coordinate and supervise the implementation of the Land Planning.

  • Identify opportunities and barriers to development.

  • Monitor and evaluate the implementation of programs of Towns and Villages organized.

  • Manage the development of residential areas.

  • Address the application to change the use of the compound, combination / separation of the compound.

  • Collect information research and market trends Land.

  • Verify records of research and putting it on the computer

  • Receive prayer and appreciation under the supervision of a registered Appraiser

  • inspect, test and harmonization value of buildings and land for the record (Data Bank)

  • Make appreciation of compensation payments, house rent, mortgages, insurance, balance (Balance sheet) and exports mal

  • Preparing drawings of diagnosis (Description diagrams)

  • Receive and review aerial photographs from the contractor.

  • Make measurement, calculation and prepare the work (Demarcation, coordination, computation and compilation).

  • Drawing a plan of testing (Survey plan)

  • Drawing a plan of document (Deed plan)

  • Incorporate quantitative information on the computer (alpha numeric data)

  • Inspect the work of surveying and incorporate information on computational work certified.

  • Make periodic images (aerial triangulation and block adjustment)

  • Prepare troops for updating maps (map revision)

  • Keeping records of aerial photographs

  • Manage and take tests tide gauge (Hydrographic survey)

  • Working outside the office (field survey operations) under the supervision of a registered surveyor.

  • Provide customer service (customer services)

  • Inspect measurement issues in the District councils and counties (technical auditing)

  • Receiving and processing applications for quantitative image space.

  • Make preparations for testing the water.

  • Analyze and explore various information (data analysis)

  • Manage testing memory (data bank)

  • Analyze and examine the results of the work of surveying and preparation of technical information.

  • Manage the production system to a computer map.

  • To advise the Board on matters of surveying and preparing the map.

  • Inspect the work of surveying and submit them to the Director of Surveying and Mapping

  • Make innovative new map

  • Provide advice to clients for specific maps (thematic map)

  • Make periodic captaincy

  • Perform data analysis (data processing and analysis)

  • Develop quantitative score (survey plan beacons) \

  • Planning and organizing camps needs assessment, measurement equipment and general requirements.

  • Preparing and analyzing equipment for the preparation of the map.

  • Analyze, sewing, cutting and pulling the printed documents.

Matangazo

  • TANGAZO LA MAFUNZO UBORESHAJI WA DAFTARI KWA WALIOFAULU USAILI January 18, 2025
  • TANGAZO LA KAZI KUKIMBIZA MWENGE WA UHURU April 11, 2025
  • KUITWA KWENYE USAILI DAFTARI LA MPIGA KURA 2024 January 09, 2025
  • TANGAZO LA UCHAGUZI September 16, 2024
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • MHE. SAWALA AWATAKA WAFANYAKAZI WA MTWARA KUIPENDA MTWARA

    May 01, 2025
  • DED KAFUNDA AWAASA MAAFISA WAANDIKISHAJI WASAIDIZI NGAZI YA KATA KWENDA KUFANYA KAZI KWA WELEDI

    January 22, 2025
  • KATIBU WA CCM MKOA WA MTWARA APONGEZA USIMAMIZI WA MIRADI YA ZAIDI YA MILIONI 800 MTWARA DC

    January 07, 2025
  • KATIBU WA CCM MKOA WA MTWARA APONGEZA USIMAMIZI WA MIRADI YA ZAIDI YA MILIONI 800 MTWARA DC

    January 07, 2025
  • Angalia Zote

Video

RC Mtwara ataka mabadiliko Ligula Hospitali
Video zaidi

Kurasa za Haraka

  • New Projects
  • Speeches
  • Organizational Structure
  • Tenders
  • Applications Forms

Kurasa Mashuhuri

  • Tanzania Government Website
  • PO-RAG
  • Public Service Management
  • Mtwara Region Office
  • Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma
  • Tovuti ya Ikulu

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Sehemu

Wasiliana nasi

    Mtwara.

    Anuani ya posta: 528.

    Simu ya Mezani: 023-2333928

    Simu: 023-2333928

    Barua pepe: dedmtwara@mtwaradc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Usiri
    • Kanusho
    • Maswali
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Copyright ©2023 MTWARA DC . All rights reserved.