Na Afisa habari.
Usimamizi bora wa sheria na kanuni za fedha umeiwezesha halmashauri ya wilaya ya mtwara kupaa katika ukusanyaji wa mapato kutoa bilioni 1.4 mwaka 2015 hadi bilioni 2.5 mwaka 2020 na hivyo ongezeko kuwa zaidi ya asilimia 10 kila mwaka ndani ya miaka mitano.
Taarifa hiyo imeelezwa na afisa mipango Thomas Luambano aliyewasilisha kwa niaba ya mkurugenzi mtendaji mbele ya waheshimiwa madiwani na wataalamu wa sekretarieti ya mkoa katika mkutano maalumu wa baraza la madiwani uliofanyika mkunwa tarehe 09 Juni mwaka huu.
Aliendelea kusema kuwa, kwa kipindi cha miaka mitano 2015 hadi 2020 halmashauri ilikisia kukusanya jumla ya Tzs. 11,914,571,378.00 ambapo hadi Juni mwaka huu imefanikiwa kukusanya Tzs. 10,546,986,455.45 ambapo ni wastani wa asilimia 89 kwa kila mwaka huku mwaka wa fedha 2018/2019 mapato yalivuka lengo na kufikia asilimia 102.6.
Aidha mkurugenzi mtendaji Qs. Omari J. Kipanga, aliongeza kuwa mafanikio hayo ni matokeo ya wataalam na waheshimiwa kufanya kazi kwa ushirikiano ambapo ulisaidia kufanya ubunifu wa vyanzo vipya vya mapato na kutekeleza miradi ya kimkakati kama vile ujenzi wa soko la samaki la msanga mkuu, pamoja na matumizi sahihi ya mfumo wa makusanyo kupitia mashine za kielektroniki “POS”.
Kuimarika kwa mapato kumesaidia upatikanaji wa mikopo ya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu, utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa jamii na kuimarisha mfumo wa uwezeshaji wananchi kiuchumi.
Pamoja na ongezeko la mapato ya ndani, waheshimiwa madiwani kupitia kwa mwenyekiti alhaji Mussa S. Ndazigula amemshukuru mkurugenzi kwa ushirikiano, uvumilivu na usikivu alioonesha kwa kipindi chote cha usimamizi na kuiongoza taasisi, mfano mzuri ni upatikanaji wa Hati Safi kupitia taarifa ya mkaguzi wa mahesabu ya serikali.
Mtwara.
Anuani ya posta: 528.
Simu ya Mezani: 023-2333928
Simu: 023-2333928
Barua pepe: dedmtwara@mtwaradc.go.tz
Copyright ©2023 MTWARA DC . All rights reserved.