Mapema leo February 18, 2023 Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe. Hanafi Msabaha amefanya ziara ya kukagua miradi itakayopitiwa na Mwenge wa Uhuru 2023 katika Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara.
Miradi hiyo yenye thamani ya Zaidi ya Tsh. Bil 2.2 ndio miradi iliyopendekezwa kupitiwa na Mwenge wa Uhuru 2023.
Aidha miradi hiyo ni pamoja na Shamba la Mikorosho lililopo Kijiji cha Mayaya kata ya Madimba lenye Thamani ya Tsh. Milioni 150,000,000/= Pesa kutoka kwa Wananchi.
Mradi wa Maji uliopo Kijiji cha Mwindi kata ya Mbawala wenye thamani ya Tsh. Milioni 800,000,000/= pesa iliyopatikana kutoka Serikali Kuu.
Mradi wa Bweni la Wasichama wenye mahitaji maalumu lililopo Kijiji cha Nanguruwe kata ya Nanguruwe mradi huu unathamani ya Tsh. Milioni 100,000,000/= pesa kutoka Serikali Kuu.
Aidha mradi mwingine ni Pamoja na Barabaara yenye urefu wa KM 1.7 Nanguruwe – Mkunwa mradi wenye thamani ya Tsh. Milion 949,139,000/= pesa iliyotolewa na Serikali Kuu.
Mradi wa Mwisho ni mradi wa ufugaji wa kuku uliopo Kijiji cha Hiyari kata ya Mayanga wenye mradi wenye thamani ya Tsh.180,000,000/= pesa za wananchi.
Aidha baada ya kusikiliza taarifa mbalimbali za miradi hiyo Mhe. Msabaha aliagiza ukamilifu wa Document zote kabla ya kufikia siku ya mapokezi ya mwenge wa Uhuru. Pia alitaka kuwepo na hesabu kamili ya nini kimefanyika .
Mwisho aliwaomba viongozi wa kata na Vijiji kusaidia utoaji wa hamasa kwa Wananchi na kushirikishwa wadau wote vikiwemo vyama vyote vya siasa kwa ujumla wake.
Mtwara.
Anuani ya posta: 528.
Simu ya Mezani: 023-2333928
Simu: 023-2333928
Barua pepe: dedmtwara@mtwaradc.go.tz
Copyright ©2023 MTWARA DC . All rights reserved.