Halmashauri ina eneo la bahari kwa upande wa mashariki lenye urefu wa km 125 na vijiji 25, ambapo wakazi wake wanategemea shughuli za uvuvi kama chanzo kikuu cha kuingiza mapato ya kila siku, wavuvi walio wengi bado wanatumia uvuvi wa kawaida kutokana na kukosa zana bora na za kisasa.
kutokana na hilo serikali imeendelea kutoa mikopo kwa vikundi vya wavuvi, pamoja na kuwashawishi wadau mbalimbali wa maendeleo kuwekeza katika sekta hiyo kwa kushirikiana na wavuvi hao kwakuwa sehemu kubwa ya Samaki wanaotumika Mtwara mjini na baadhi ya wilaya zinazopakana nazo wanavuliwa katika ukanda huu.
Eneo la mwambao wa pwani linatumika kwa shughuli za Uvuvi ambapo kwa mwaka 2017 jumla ya kg. 629,100 za samaki zilivuliwa na kutumika, wengi wa samaki hawa wanatumika kwaajili ya matumizi ya nyumbani kupitia wachuuzi wanaonunua kwa minada kisha kuuza kwa kuwatembeza mtaani, asilimia ndogo sana wananunuliwa kisha kusafirishwa sehemu mbalimbali nadani na nje ya mkoa.
Ili kuongeza uzalishaji wa samaki na kuleta uwiano wa uzalishaji, halmashauri imeendelea kutoa elimu kwa wananchi wake kwa kuwashawishi kuanzisha ufugaji wa samaki kwa kutumia mabwawa ya kuchimba, ingawa mwanzoni ilikuwa ngumu kuelewkea lakini kwa sasa kuna kasi kubwa ya ufugaji wa samaki baada ya kuona faida inayopatikana, samaki wanaofugwa na kupendwa na wanunuzi ni Sato, Changu na Mwatiko ambao wameonesha kupata soko kubwa kwa sasa.
Kwa sasa hakuna uwekezaji mkubwa uliofanyika katika sekta hiyo isipokuwa mialo inayotumika na serikali kwaajili ya kukusanya mapato, kuna fursa kubwa ya uwekezaji wa viwanda vya kusindika minofu ya samaki katika eneo la Mtwara Vijijini kwakuwa eneo lililotengwa kwaajili ya viwanda vya usindikaji lipo na limeshapimwa, malighafi kwaajili ya kusidika yapo ya kutosha, nishati kwaajili ya kuendesha mitambo ya viwanda ipo ya kutosha ikiwemo na gesi asilia, vilevile kuna miundo mbinu bora kwaajili ya kusafirisha bidhaa kwaajili ya masoko.
Mtwara.
Anuani ya posta: 528.
Simu ya Mezani: 023-2333928
Simu: 023-2333928
Barua pepe: dedmtwara@mtwaradc.go.tz
Copyright ©2023 MTWARA DC . All rights reserved.