Na Afisa habari.
Mtandao wa asasi zisizo za kiserikali mkoani mtwara (MTWANGONET) leo 22/05/2020 limezindua kampeni kabambe ya uhamasishaji wa kujikinga dhidi ya maambukizi ya virusi vya CORONA katika ukumbi wa mikutano wa Shule ya Msingi Msijute, halmashauri ya wilaya ya Mtwara.
Akitolea maelezo mafupi ya kampeni hiyo, mratibu wa mtwangonet, bi. Fidea Ruanda amebainisha kuwa, elimu itakayotolewa ni shirikishi, ikilenga kuleta uelewa mpana juu ya kujikinga na CORONA, kuamsha ari kwa wadau wengine kujitokea katika kuielimisha jamii ili kuondoa dhana ya kuiachia serikali peke yake..
Aliendelea kusema kuwa, mradi huo utadumu kwa miezi mitatu kuanzia mwezi Mei hadi Julai mwaka huu kulingana na mpango na bajeti yake ukilenga kufanya hamasa katika kata nane za halmashauri ya wilaya ya mtwara zenye wakazi zaidi ya elfu 40 ambapo amezitaja kata hizo kuwa ni Tangazo, Madimba, Moma, Nalingu, Mbawala, Nanguruwe, Naumbu na Kitere.
Pamoja na matumizi ya wataalamu katika kutoa hamasa, kampeni hiyo itachagizwa na kutoa elimu kwa njia ya vyombo vya habari, kutumia ujumbe mfupi wa meseji za kawaida katika simu za mikononi, kuchapisha mafulana yatakayogawiwa kwa vikosi kazi vya watu kumi kila kata ambao watasaidia kutoa elimu ya kujikinga na virusi vya corona.
Aidha, kikao hicho cha uzinduzi kilihudhuriwa na waheshimiwa madiwani kutoka kata zote nane na wataalamu saba ambapo walilishukuru shirika hilo kwa kuamua kujitoa kusaidia mapambano dhidi ya corona, wameshauri kulifikia kundi la waalimu kwa minajili ya kuwapa elimu ambayo itasaidia katika kuwakinga watoto wa shule pindi zitakapofunguliwa.
Akiongea kwa niaba ya waheshimiwa madiwani, mwenyekiti wa halamsahauri mhe. Mussa S. Ndazigula aliendelea kuishukuru mtwangonet kwa kuwa wawazi na kushirikisha wadau muhimu, ameutaka mradi huo uwafikie pia waumini wa dini zote mbili kwakuwa katika maeneo yao ya kumuomba Mungu yanakutanisha watu wengi wenye kutoka sehemu tofauti.
Mtwara.
Anuani ya posta: 528.
Simu ya Mezani: 023-2333928
Simu: 023-2333928
Barua pepe: Mtwaradc@mtwara.go.tz
Copyright ©2020 MTWARA DC . All rights reserved.