MKUU WA MKOA WA MTWARA ARIDHISHWA NA MRADI WA UJENZI WA SHULE YA SEKONDARI LYOWA
Leo Disemba 18,2023 Mhe.Col Ahmed Abbas Mkuu wa Mkoa wa Mtwara akiwa ameambatana na kamati ya ulinzi na usalama Mkoa alifanya ziara ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo katika Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara.
Katika ziara hiyo Mhe. Abbas ametembelea ujenzi wa shule mpya ya Msingi Umoja iliyopo katika Kijiji cha Kinyamu Kata ya Dihimba inayojengwa kwa gharama ya sh. Million 331.6 kupitia mradi wa BOOST pamoja na shule mpya mbili za Sekondari Muungano na Lyowa zinazojengwa kwa gharama ya sh.million 560.5 na million 497.4 kupitia mradi wa SEQUIP.
Akiongea mbele ya wananchi Mhe. Col Abbasi alisema kuwa madhumuni ya kukagua utekelezaji wa miradi hii ya ujenzi wa shule ni kupima kama Januari kunauwezekano wa kuingia wanafunzi.
“Natumia fursa hii kuwapongeza kwa kazi nzuri na yenye viwango kwani hata kwa macho inaonekana” aliongeza Mkuu wa Mkoa.
Wakati huo huo Mkuu wa Mkoa amemtaka Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara kugeuza changamoto kuwa fursa na kusisitiza kama mzabuni haendani na kasi ya ujenzi basi abadilishwe.
Mtwara.
Anuani ya posta: 528.
Simu ya Mezani: 023-2333928
Simu: 023-2333928
Barua pepe: dedmtwara@mtwaradc.go.tz
Copyright ©2023 MTWARA DC . All rights reserved.