Mkutano wa Baraza la Madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara umeendelea tena leo Mei 4, 2023, katika ukumbi wa Shule ya Sekondari Mustafa Sabodo ambapo hoja mbalimbali zilijadiliwa na kupatiwa ufumbuzi.
Akizungumza mbele ya wajumbe wa baraza Mhe. Saidi Abdallah Makame, makamo Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara alisema, Serikali imeleta miradi mingi hivyo Madiwani pamoja na Watendaji wa Kata wasimamie vizuri miradi ya maendeleo ili miradi inayotekelezwa iende kwa wakati na ilete tija.
“Najua kunachangamoto baadhi ya maeneo Wananchi kutoshiriki vizuri katika miradi ya maendeleo, hivyo kunajukumu kubwa la kwenda kusimamia maeneo hayo ili miradi inayotekelezwa kwenye maeneo yetu iende kwa wakati na ilete tija” aliongeza kaimu Mwenyekiti huyo.
Akitoa salamu za Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Katibu Tawala wa Wilaya ya Mtwara Ndg. Thomas Salala alisema Mhe. DC anakumbusha watendaji wote kuanzia Waheshimiwa Madiwani, wakuu wa idara, watendaji wa Kata/Vijiji na maafisa Tarafa wote kufanya usimamizi wa pamoja wa miradi ya maendeleo.
Ndugu Thomas Salala alimaliza kwa kuwaomba watendaji waendelee kushirikiana ili miradi ambayo Serikali imeleta imalizike kwa wakati na ilete tija.
Mtwara.
Anuani ya posta: 528.
Simu ya Mezani: 023-2333928
Simu: 023-2333928
Barua pepe: dedmtwara@mtwaradc.go.tz
Copyright ©2023 MTWARA DC . All rights reserved.